Uupate usaidizi wapi?
Unashauriwa kuutafuta usaidizi unapokuwa na changamoto za masuala ya afya ya akili. Katika video hii, utasikia aina ya usaidizi unaoweza kuupata katika Ufini. Katika Ufini, unaweza kuwaamini wataalamu.
Tazama inayofuatia: Imarisha afya ya akili
Unataka kujua zaidi?
Matibabu ya kisaikologia ni tiba ya afya ya akili. Katika matibabu ya kisaikologia, mgonjwa huzungumza na mtaalamu kuhusu mawazo, hisia na matatizo kisiri. Mazungumzo haya huyaponya na husaidia kuyashinda mambo magumu.